Monday, January 30, 2012

HII INAUKWELI WA KUTOSHA TU

Wanawake walio wengi hawajui namba za magari yao, ni kitu cha kushangaza ,kidogo lakini ni muhimu sana ila ukweli ndo huo, wanawake ufahamu magari yao kwa alama tu kwa mfano kama aliichubua hiyo ndo itakuwa alama yake, ama kama ina 'tintedi' na ikitokea akajua namba basi ata jua T...WHD namba za kati hazijui na akijua namba za kati herufi hazijui

Ukija kwenye swala   service ya gari pia mpaka akumbushwe na mume, kaka ama mtu wa karibu sana ambaye lazima utakuta ni mwanaume bisha au kubali ila ndo iko hivyo

Kitu kama maji pia anaweza asijue kama gari yake ina maji au haina au hata pa kuweka hapajui na maji anayo ya akiba ndo utakuta anamsimamisha kijana mpita njia kumsaidia na kumlipa

Yaani haya mambo ya magari huleta stress kweli kwa kinadada hasa inapopmgomea ghafla.....

No comments:

Post a Comment