Monday, August 1, 2011

UTAKUBALIANA NA MIMI KUWA MTOTO NI MKWELI KWA KILA TUKIO KWAKE

Anapofurahi, huwa na furaha ya kweli toka moyoni na wakati mwengine huwa anaamua kufurahi mwenyewe tu mpaka ma wewe inatokea unafurahi,tofauti na sisi watu wazima.

Akilia analia kweli na umemuuzi  kweli au kuna kitu anachohitaji unamzuia kukipata/kukifikia,sio sisi watu wazima wakati mweninge tunalia ili watu wapate kuhadithia kwamba umelia.

Akikasirika mtoto anakasirika kweli wala haigizi unaweza ukaliona hili kwa uso wake tu, sio sisi watu wazima huwa tunatabia ya kujiandaa kukasirika yaani unaitafuta sababu mapemaaaa ili ukasirike.

Akifanyiwa kitu kikamuuma  kinamuuma kweli hasa katika umri huu hato sahau mpaka anapoacha dunia hii, lakini sisi watu wazima ukiona umeumia hivi ni jambo la mapenzi tu hilo amabalo unatokea kulisahau pindi tu unapopata mtu mpya/mbadala/suluhu.

Ku-bore-ka kupo hata kwa watoto, nadhani sehemu hii ndo huwa labda tunafanana  kwa kweli. I WISH MIMI, WEWE, YULE TUNGEKUWA WAKWELI KAMA WATOTO.

No comments:

Post a Comment