Tuesday, August 9, 2011

UKISTAAJABU YA MUSA UTAYAONA YA FIRAUNI ...........

Leo Asubuhi ,nikiwa njiani kuelekea kazini, huwa mara nyingi napenda kusikiliza radio mabali mbali ili kujua vitu mbalimbali, Mara  nikasikia Bonge wa Clouds fm anaripoti kwamba kinondoni Block 41 kuna mamba,mhm ...kuna mamba ametoka wapi? imekuwaje?tangu lini? nikajiuliza maswali mengi bila majibu mwisho wasiku nikakubali tu kwamba kuna mamba kinondoni,
Kuna kibwawa kidogo maeneo hayo ya Block 41 kipo kwa bondeni hivi ndo kuna mamba hapo yapata miaka miwili hivi, wananchi wa maeneo hayo wamesharipoti sehemu zote husika lakini mali aslili wamesema watakuja kumchukua mpaka sasa umefika mwaka wa pili! wenyewe wanasema jua likianza kuchomoza anatoka anapanda kwenye kichuguu anaota jua mpaka anakapoona  limemtosha.
HA HA HA UKISIKIA HABARI HII KWA HARAKA UTASHAANGAA NA KUJIULIZA SANA KAMA MIMI, KISIKIA BLOCK 41 KUNA MAMBA.

No comments:

Post a Comment