Wednesday, July 20, 2011

KATIKA MAHUSIANO USIPOKUWA MAKINI UTAKUWA NI MTU WA KULIA NA KUUMIZWA KILA WAKATI.....

Inawezekana usiamini macho yako kwa kile kilichotokea kwa yule unayempenda,labda ulimfumania,na mwanamke mwingine,,hivyo kujikuta ukilia kwa uchungu usiamini kilichotokea na katika hatua hii ndio wengine unakuta anafikia uamuzi wa kusema kila mwanamume ni muongo na siwezi kupenda tena

Maumivu huwa yanatofautiana mwingine hufika hatua ya kuugua na hata kulazwa hospitali,mwingine kunywa sumu..yote ikiwa ni kukata tamaa ya kuendelea kuishi kwasababu ya mapenzi..jamani mapenzi ni matamu sana lakini yanaweza kugeuka na kuwa machungu,,,bila kutegemea..kilichobaki ni kufanya maamuzi sahihi pale unapotafuta mchumba kuwa makini sana usikurupuke na kujikuta siku zote wewe ni mtu wa kulia katika mapenzi.Utakuta ndani ya mwaka mmoja umekuwa katika mahusiano na watu zaidi ya wa tano na wote wakakuumiza..yaani unajikuta umekuwa kama chombo cha kutumika na kutupwa.Umakini ni wa muhimu sana.

No comments:

Post a Comment