Wednesday, July 27, 2011

SIO KILA MTU ANAFURAHIA KUONA MNAPENDANA

Ni wazi kabisa kuwa wawili wakipendana na kuwa pamoja,kuna baadhi ya watu huwa na wivu na chuki zisizo na msingi ambapo unapoona mwenzako yuko kwenye mahusiana na mtu anayempenda,

anamjali na muda wote wapo katika furaha na huku akiangalia kwa upande wake mahusiano aliyonayo hakuna amani basi akiona mwenzake mahusiano yake yapo vizuri anachukia na kuwaza afanye nini ili aweze kuvuruga uhusiano huo
hapo ndipo ataanza kutafuta maneno ya uongo na kukuletea alimradi tu awakorofishe usipokuwa makini utajikuta unakuwa katika migogoro.

Muhimu kuchunguza kile unachoambiwa, kwani siyo wote wanapenda kukuona ukiwa na furaha.Kitu kingine ni kwamba kwa wale wenye tabia ya kuwa na chuki binafsi haipendezi kumfanyia mwenzio vibaya ni vizuri kutamani na kuwa na malengo ya kuitafuta furaha kama aliyonayo mwenzio kuliko kuchukia na kutaka kumuharibia kwani kwa kufanya hivyo haikusaidii chochote. Jamani tuwe makini kwani ni vigumu kumtambua adui yako inawezekana akawa ndugu yako,rafiki yako au jirani yako ......

1 comment:

  1. its true mom u hav to be care on what unachoambiwa...gud thing dont last long

    ReplyDelete