Wednesday, October 26, 2011

IMETOSHA WENZANGU


Tabu maisha kila siku,maajabu mchana hata usiku haya ndo maisha yetu

Salama sana wenzangu, leo hizi ni salamu zangu za dhati, salamu za upendo salamu zitokazo ndani uvunguni mwa moyo wangu salamu zilizobeba dhati ya moyo wangu,nyoyo zetu zimebeba chuki , visasi na risasi,Nafsi zetu zinatiririka  machozi ya majuto na upendo machozi haya yameanza safari ndefu yakilainisha pua zilizo tuonea kinyaa kila tulipopaza sauti, ikilainisha midomo iliyotubeza kutununia na kutufokea yakitiririka zaidi hadi kifuani kulainisha mioyo migumu,tena zaidi machozi inalainisha mikono migumu iliyotusukumia mbali sasa inatukumbatia na kufungua ukurasa mpya.Isikieni sauti yangu ikiwanong'oneza turudishe mioyo yetu nyuma, Furaha yetu kamili inategemea furaha yao poleni wenzangu nawatakia maisha yenye furaha.YA JANA NI HISTORIA, YA LEO NI MAJAALIWA NA KESHO NI NDOTO TUNAYOITEGEMEA KUTOKA KWA MUNGU.

No comments:

Post a Comment