Tuesday, September 27, 2011

MALE/FEMALE MIDLIFE CRISIS

Nilikuwa nasoma soma articles mbalimbali nikakutana na jambo hili baada ya kusoma nikagundua ni la muhimu sana kufahamu.Sijui namna ya kuuiita MALE MIDLIFE CRISIS kwa kiswahili ila nimefahamu yafuatayo.
Ni kipindi ambacho mwanaume anajiuliza maswali mengi kuhusu maisha yake na kutokuridhishwa na mengi yanayoendelea.Hiki ndio nimekifanyia kazi kwa ujana wangu?hiki ndio nilitarajia kupata wakati nimekuwa mwanaume?Hapo inakuwa mbaya zaidi kama hajatimiza malengo yake.Ubaya unakuja bila wao kujua uchungu wote wa kutokutimiza malengo anauhamishia kwa mkewe.
Atatoka na kwenda kufanya vitu vitakavyomfanya ajihisi yeye bado kijana na matumaini mapya.Hapo ndio wengine hutelekeza familia zao,kulewa,kubadili wanawake kama nguo tena vibinti vidogo.Matokea hapo yanakuja atafilisika pesa itaishi na kuzidi kudidimia na kusambaratisha familia.
Haya yote yanatokea kwa sababu wanaume wamefundishwa kukaa kimya kufa na tai shingoni lakini haitakiwi kuwa hivyo....zungumza.
Hiki ni kipindi kibaya sana kwa wanaume wengi kwenye stage hii huweza kuishia kujiua.

Na ili kumsaidia mwanaume kama huyu lazima mke ujue tatizo ni hili na umsupport badala ya kupigizana nae kelele.Kivipi sasa?
 Hii habari nimeitoa kwa blog ya Dina marious, nimeisoma nikaona hiki ni kitu cha msingi ambacho ni cha kweli na kinasumbua hasa, ndo nikataka kujua kama na kwa wamawake ipo hii?

Nikagundua kuwa na kwa wanawake ipo pia lakini kuna utofauti kidogo, mwanamke inaweza mpata kutokana na mambo  haya :MABADILIKO YA UMBILE NA IKATOKEA AKACHUKIA          MABADILIKO HAYO
                                     :AMA AKAONA ANAFANYA KAZI KWA BIDII NA NGUVU SANA LAKINI HAONI MAFANIKIO YA KAZI HIYO
    Na vitu vidogo vidogo vingi lakini woe kati ya mwanamke ma mwanaume wanapitia stage moja ya kupata

  • Shock
  • Denial
  • Depression
  • Anger
  • Acceptance

No comments:

Post a Comment