Wednesday, August 10, 2011

MR BEAN APATA AJALI

Mchekeshaji Rowan Atkinson aka Mr. Bean, apata ajali ya gari na kuharibu gari yake yenye thamani ya £650,000, sport car hiyo imeharibika sehumu kubwa kwa mbele na upande wa milango, lakini mwenyewe ameumia kidogo tu.


Mzigo ndo huo tena

Tuesday, August 9, 2011

UKISTAAJABU YA MUSA UTAYAONA YA FIRAUNI ...........

Leo Asubuhi ,nikiwa njiani kuelekea kazini, huwa mara nyingi napenda kusikiliza radio mabali mbali ili kujua vitu mbalimbali, Mara  nikasikia Bonge wa Clouds fm anaripoti kwamba kinondoni Block 41 kuna mamba,mhm ...kuna mamba ametoka wapi? imekuwaje?tangu lini? nikajiuliza maswali mengi bila majibu mwisho wasiku nikakubali tu kwamba kuna mamba kinondoni,
Kuna kibwawa kidogo maeneo hayo ya Block 41 kipo kwa bondeni hivi ndo kuna mamba hapo yapata miaka miwili hivi, wananchi wa maeneo hayo wamesharipoti sehemu zote husika lakini mali aslili wamesema watakuja kumchukua mpaka sasa umefika mwaka wa pili! wenyewe wanasema jua likianza kuchomoza anatoka anapanda kwenye kichuguu anaota jua mpaka anakapoona  limemtosha.
HA HA HA UKISIKIA HABARI HII KWA HARAKA UTASHAANGAA NA KUJIULIZA SANA KAMA MIMI, KISIKIA BLOCK 41 KUNA MAMBA.

REST IN PEACE SAM LOCO EFE

Habari za huzuni na za kushtua zimelikumba soko la burudani ya filamu nchini Nigeria na Afrika kwa ujumla baada ya kuondokewa na mtu muhimu na anayekubalika kwa kazi zake katika Tasnia ya Uigizaji.
Sam  loco efe ambaye ni comedian mzuri tu amefariki juzi akiwa chumbani kwake( hotelini) walipokuwa wameenda kurecord movie yao mpya. Mbali na uigizaji pia alikuwa mtunzi, mwandishi wa script na ni muimbaji pia na anatambulika kama mmoja ya watu muhimu katika movie ya THING FALL APART ,wengi wetu tunaijua enzi za secondary.
MUNGU AILAZE ROHO YA SAM LOCO EFE MAHARI PEMA PEPONI , AMINA

OUR BROTHER AAMUA KUMEREMETA NA KIPENZI CHAKE

NEW, couple in town, MR & MRS NYEMBERA

PATRICK NA MKEWE AGNESS WALIPOKUWA WANAONGE NA E-NEWS HAPO

KARIBU WIFI YETU.......................
WADADA TULIKUWEPO KUSHEHEREKEA NA KAKA YETU

>
MWENDO ULIKUA KWAITO TU AIDHA UNAJUA AU HAUJUI.............

Monday, August 1, 2011

THE ROYAL WEDDING

Uti Nwachukwu and Munachi Abii’s


                                                         
                                                  Wenye wivu wajinyonge wenyeweeeeeeeee

Ukweli ni kwamba hawa sio wanandoa wala wapenzi, walikuwa wakipiga picha kama wanamitindo kwa ajili ya uzinduzi wa jarida la  mamabo ya harusi huko kwao naija.

UTAKUBALIANA NA MIMI KUWA MTOTO NI MKWELI KWA KILA TUKIO KWAKE

Anapofurahi, huwa na furaha ya kweli toka moyoni na wakati mwengine huwa anaamua kufurahi mwenyewe tu mpaka ma wewe inatokea unafurahi,tofauti na sisi watu wazima.

Akilia analia kweli na umemuuzi  kweli au kuna kitu anachohitaji unamzuia kukipata/kukifikia,sio sisi watu wazima wakati mweninge tunalia ili watu wapate kuhadithia kwamba umelia.

Akikasirika mtoto anakasirika kweli wala haigizi unaweza ukaliona hili kwa uso wake tu, sio sisi watu wazima huwa tunatabia ya kujiandaa kukasirika yaani unaitafuta sababu mapemaaaa ili ukasirike.

Akifanyiwa kitu kikamuuma  kinamuuma kweli hasa katika umri huu hato sahau mpaka anapoacha dunia hii, lakini sisi watu wazima ukiona umeumia hivi ni jambo la mapenzi tu hilo amabalo unatokea kulisahau pindi tu unapopata mtu mpya/mbadala/suluhu.

Ku-bore-ka kupo hata kwa watoto, nadhani sehemu hii ndo huwa labda tunafanana  kwa kweli. I WISH MIMI, WEWE, YULE TUNGEKUWA WAKWELI KAMA WATOTO.

NAWATAKIA KHERI YA RAMADHAN WOTE MLIOJAALIWA KUFUNGA

Amina
Tuzingatie tunayotakiwa kufanya, na tuache tusiyotakiwa kufanya.