Monday, April 9, 2012

MHESHIMIWA RAIS JAKAYA KIKWETE ALIPOENDA KUTOA POLE KWENYE MSIBA WA KANUMBA

Alipokuwa anajaza kitabu cha wahudhuriaji/waombolezaji

Akisalimiana na baadhi ya wasanii waliokuwepo  msibani



Saturday, April 7, 2012

MAMBO YANAYOENDELEA NYUMBANI KWA KANUMBA

Mdogo wake na marehemu Kanumba akiongea na waandishi wa habari

Picha iliyoko sebuleni kwa kanumba

Vitu vimetolewa ili watu waweze kukaa vizuri msibani

Jackline Wolper akiwa amezimia

Baadhi ya waombolezaji

Friday, April 6, 2012

HIZI NI BAADHI YA PICHA ZA MSIBANI HUKO SINZA NYUMABNI KWA KANUMBA





REST IN PEACE KANUMBA

Mungu ailaze roho ya marehemu STEVEN KANUMBA mahara pema peponi

R.I.P

HAKIKA HILI LINANIKWAZA SANA

Kuna baadhi ya vitu huwa vinaniumiza  sana kichwa pengine kutokana na udhaifu wa moyo wangu au huruma ya moyo wangu au sijui ni Maisha tu, maana huwa nalaumu, mara naona sina haki ya kulaumu....yaani sijui kwa nini!

Hivi , naomba niulize swali hili kwa  kaka zangu wapendwa, huwa mnawaza nini mnapoa mua kufanya mapenzi na wanawake wenye matatizo ya akili,mnawapa mimba wanateseka, wanazaa watoto wanateseka, mwisho wanakuja kuwa watoto wa mitaani, majambazi na vijana wasiofaa , huwa mnaanza kurifikiria hili kabla hamjatenda unyama huo?

Mlishawahi sikumoja kujuta juu ya mambo machavu na yakinyama mnayo yafanya kweli? umeshawahi kufikiria basi kuchukua jukumu la kulea mtoto uliyemsababisha? hakika huu ni unyama

Au huwa mnaona raha tu wakati huo wa kufanya unyama wenu,bila kujua tendo unalolifanya ni la kikatili na linamatokeo makubwa?

Hivi unajua kuna mimba zinataabu sana na zina kuja na mambo mengi ikiwemo magonjwa na kadharika au kwa kuwa unaona mwanamke ni kichaa basi ataishi kwa nguvu za mungu! umefikiria thamani yake ya utu kweli!

Ona sasa haya ndo matokeo unayoleta hapa dunia unatengeneza roho za chuki kwa binadamu, huyu mtoto hata kaa apende mtu wala kujua thamani ya binadamu kwa kuwa haiko hivyo kwake, unajua hilo?


Tafadhari, kama umefanya hivyo juta, uombe msamaha kwa Mwenyezi Mungu na ufuate damu yako huko uliko iacha kwa kweli.