Wednesday, September 28, 2011

BECAUSE IM ADDICTED!

Maisha lazima yaendeleeeeeeeeeeeeeee

HAWA NDO NAWAFEEL ILE MBAYA KWENYE MEDIA SASA HI VI KWA UPANDE WA TV

Fatma Almasi Nyangasa wa ITV

Godwin Gondwe wa ITV

Zamaradi mketema wa CLOUDS TV

Ivon Msemembo wa ITV
Na wengine ni Enock mwijane wa TBC pamoja na Joan Itanisa wa STAR TV, hawa nimeshindwa kupata picha zao.
Kiukweli hawa wanaivutia kwa kazi zao na muonekano wao, unapoangalia vipindi vyao unajua nini wanafanya kwa kuwa wanakupa information za kutosha na za kueleweka, wanajiamini kupitiliza wanapendeza yaani hawa nawakubali kiukweli.
NOTE: Wapo wengine ninaowakubali lakini sijaweweka kwa kuwa ni sehemu ninayofanyia kazi watu wasije ona napendelea bure.......................nitakuletea na wa redio kwa siku nyengine.

Tuesday, September 27, 2011

MALE/FEMALE MIDLIFE CRISIS

Nilikuwa nasoma soma articles mbalimbali nikakutana na jambo hili baada ya kusoma nikagundua ni la muhimu sana kufahamu.Sijui namna ya kuuiita MALE MIDLIFE CRISIS kwa kiswahili ila nimefahamu yafuatayo.
Ni kipindi ambacho mwanaume anajiuliza maswali mengi kuhusu maisha yake na kutokuridhishwa na mengi yanayoendelea.Hiki ndio nimekifanyia kazi kwa ujana wangu?hiki ndio nilitarajia kupata wakati nimekuwa mwanaume?Hapo inakuwa mbaya zaidi kama hajatimiza malengo yake.Ubaya unakuja bila wao kujua uchungu wote wa kutokutimiza malengo anauhamishia kwa mkewe.
Atatoka na kwenda kufanya vitu vitakavyomfanya ajihisi yeye bado kijana na matumaini mapya.Hapo ndio wengine hutelekeza familia zao,kulewa,kubadili wanawake kama nguo tena vibinti vidogo.Matokea hapo yanakuja atafilisika pesa itaishi na kuzidi kudidimia na kusambaratisha familia.
Haya yote yanatokea kwa sababu wanaume wamefundishwa kukaa kimya kufa na tai shingoni lakini haitakiwi kuwa hivyo....zungumza.
Hiki ni kipindi kibaya sana kwa wanaume wengi kwenye stage hii huweza kuishia kujiua.

Na ili kumsaidia mwanaume kama huyu lazima mke ujue tatizo ni hili na umsupport badala ya kupigizana nae kelele.Kivipi sasa?
 Hii habari nimeitoa kwa blog ya Dina marious, nimeisoma nikaona hiki ni kitu cha msingi ambacho ni cha kweli na kinasumbua hasa, ndo nikataka kujua kama na kwa wamawake ipo hii?

Nikagundua kuwa na kwa wanawake ipo pia lakini kuna utofauti kidogo, mwanamke inaweza mpata kutokana na mambo  haya :MABADILIKO YA UMBILE NA IKATOKEA AKACHUKIA          MABADILIKO HAYO
                                     :AMA AKAONA ANAFANYA KAZI KWA BIDII NA NGUVU SANA LAKINI HAONI MAFANIKIO YA KAZI HIYO
    Na vitu vidogo vidogo vingi lakini woe kati ya mwanamke ma mwanaume wanapitia stage moja ya kupata

  • Shock
  • Denial
  • Depression
  • Anger
  • Acceptance

Friday, September 23, 2011

JAMANI WALE WENZANGU NA MIMI MNAOPENDA MOVIE/SERIES ZA STORY MNAWEZA MKACHEKI NA HIZI

MOVIE

MOVIE

SERIES

HIVI NI BAADHI YA VIVAZI VILIVYONIVUTIA KUTOKA HUKO LONDON FASHION WEEK

Rangi na mtindo wa nguo kiukweli unavutia hapa ni "MUONEKANO WAKE KWA MBELE"

MUONEKANO KWA NYUMA

KWA MBELE IKO SIMPLE HII

KWA NYUMA INAKIMTINDO FRESH SANA

AS U SEE


KAMA RANGI ZINA BLOCK VILE

CHEKI CHINI YA NYAYO HAPO

NECKLESS NDO IMENIVUTIA ZAIDI HAPA

AS U SEE

                                                    The Designer, Folake Folarin-Coker

KAREN AMEAMUA KUIFIKIA JAMII SASA

By the way this is new look ya Karen katika fashion magazine

Hivi karibuni, mdada alitembelea kituo cha yatima huko mjini Jose NIGERIA na kutoa misada mbali mbali kwa watoto wa kituo hiko

                                                                     Peace and love

                                               Hawa ni baadhi ya watoto katika kituo hiko

Inavutia na kupendeza kwa watu kama hawa kuikaribia jamiii kwa ukaribu zaidi.

Wednesday, September 14, 2011

KAMATI YA MISS TANZANIA YAOMBA RADHI

TAARIFA YA KUOMBA RADHI KWA NDUGU ZETU WALIOPATWA NA MAAFA YA AJALI YA MELI HUKO ZANZIBAR KUTOKA KWA WAANDAJI WA SHINDANO LA VODACOM MISS TANZANIA –
Usiku wa kuamkia jumamosi ya tarehe 10 / 09 2011 tukio kubwa na la huzuni lilitokea huko Zanzibar ambapo wananchi wengi walipoteza maisha na wengine kujeruhiwa wakati walipopatwa na ajali ya kuzama kwa MELI iliyokuwa ikitoka Unguja kuelekea Pemba. Kwa bahati mbaya siku hiyo ya Jumamosi taaasisi yetu ilikuwa inahitimisha Fainali za Taifa za Mashindano ya Urembo ya Miss Tanzania 2011. Kama waandaaji wa Mashindano haya na wenye Mamlaka kamili ya maamuzi juu ya ama kuendelea au la kuahirisha jambo hili, tulipatwa na mshituko mkubwa sana juu ya tukio hilo. kamati yetu ilikaa na kutakafari katika tukio hilo kwa kuzingatia mambo yafuatayo:- • Taarifa kamili ya maafa haya tuliipata rasmi saa tisa na nusu mchana ( 9:30 ) siku ya jumamosi ambayo ilikuwa ni masaa machache kabla ya Fainali za Miss Tanzania kuanza katika ukumbi wa Mlimani City. • Wenzetu wa TFF waliendelea na mechi za ligi kuu ikiwemo ya Yanga na Ruvu Shooting. • Katika kumbi za starehe ikiwemo mabaa na burudani za muziki wa bendi na kumbi za disco ziliendelea kama kawaida • Muda uliokuwa umebaki kuwakilisha jina la mshiriki wetu kwenye fainali za Miss World zilikuwa zimekwisha hivyo kulikuwa na hatari ya kupoteza nafasi hiyo • Pia tamko rasmi la kusimamisha shughuli zote za burudani lilianza tarehe 11 septemba 2011 kuomboleza Kitaifa maafa hayo. Hata hivyo kama waandaaji tulifanya shindano tukiwa katika maombolezo kwani kabla ya kuanza shindano Watu wote waliokuwepo ukumbini walisimama kimya kwa dakika moja na hata washiriki walipoingia kwenye jukwaa kwa mara ya kwanza walikuwa wamevaa vitambaa vyeusi katika mikono yao ikiashilia maombolezo. Hali hii imetupa mkanganyiko na kujikuta tukiendelea na mashindano kitu ambacho tunaona tumewakosea Watanzania wenzetu. Kama Waandaaji tunapenda kusistiza kwamba tunawajibika kwa hayo yaliyotokea na si Taasisi yeyote au Kampuni yeyote na tunaomba ichukuliwe kama ni makosa ya kibinaadamu hasa ukizingatia mazingira magumu tuliyokuwa nayo kwa wakati huo na mkanganyiko wa matukio na taarifa za tatizo hilo. KUOMBA RADHI Hata hivyo shughuli hiyo inawezekana imewakwaza watu wengi na kwa sababu hiyo na pia hali halisi ya janga hilo na kwa niaba ya viongozi wenzangu na wadau wa shughuli zetu tunatoa tamko la dhati kwa Familia za ndugu wote walikumbwa na maafa haya, wale wote walionusurika katika ajali hii na Watanzania wote kwa ujumla, kwamba TUNAWAOMBA RADHI KWA MKANGANYIKO ULIOTUTOKEA HADI KUFIKIA HALI HII. Hatuna neno zaidi ya kusema na kusisitiza “TUNAOMBA RADHI” Mwenyezi MUNGU aziweke roho za marehemu mahali pema peponi, Amina,

Hashim Lundenga Mkurugenzi

THIS TIME FOR AFRICA

                                                                    Leila Lopes wins the 2011 Miss Universe crown

                                                            WOW..to Angola and Africa
                                                                        Vazi la jioni hilo

                                                          Nice picture kwa kweli


                                                            Hapa sasa.....................


                                                           Colour zime block mwenzangu!!!

Tuesday, September 13, 2011

HII NDO ILEEEEE AJALI YA NDEGE ILIYOTOKEA CONGO


Inasemekana watu kumi waliokuwa kwenye ndege walitolewa kwenye mabaki ya hiyo ndege wakiwa hai. Pia wanasema hawajui watu wangapi wamekufa waliokuwa kwenye eneo ilipoanguka. Wanasema imeanguka kwenye soko.



KENYA YAMETOKEA KAMA YALIYOWAHI KUTOKEA TANZANIA

Baadhi ya maiti zilizoungua kutokana na mlipuko wa moto kwenye Bomba la mafuta huko kenya

Mjeruhiwa huyo akikimbizwa hospitali kupata msaada wa kiafya wa haraka

HAKIKA SEPTEMBER HII HAITASAHAULIKA KWA TANZANIA

Haita sahaulika kwa sababu ya ajali kubwa mbili zilizotokea septermber 10 huko Zanzibar na Septermber 12 huko Kenya
Hawa ni baadhi ya watu waliokuwa wanasuburi msada wa kuokolewa kutoka hapo walipokuwa

Hawatakaa wasahau kamwe watu hawa

Mmoja kai ya watu aliopoteza wapendwa wake kutokana na ajali ya meli akifarijiwa  hapa

Hii ilikuwa Duwa ya kuwaombea wote waliotangulia mbele ya haki kutokana na ajali hiyo